Amos 5:10-15


10 amnamchukia yule akemeaye mahakamani,
na kumdharau yule ambaye husema kweli.


11 bMnamgandamiza maskini
na kumlazimisha awape nafaka.
Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari,
hamtaishi ndani yake;
ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu,
hamtakunywa divai yake.

12 cKwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu
na ukubwa wa dhambi zenu.

Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwa
na kuzuia haki ya maskini mahakamani.

13 Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza kimya nyakati kama hizo,
kwa kuwa nyakati ni mbaya.


14 dTafuteni mema, wala si mabaya,
ili mpate kuishi.
Ndipo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote atakuwa pamoja nanyi,
kama msemavyo yupo nanyi.

15 eYachukieni maovu, yapendeni mema;
dumisheni haki mahakamani.
Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote
atawahurumia mabaki ya Yusufu.

Copyright information for SwhKC